UTAFITI:Kuongelea baharini kunaongeza matatizo ya tumbo, masikio....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
WATAFITI wamebaini kuogelea baharini kunaongeza  kiwango kikubwa cha matatizo ya tumbo, kuumwa na masikio na magonjwa mengine.

Chuo kikuu cha matibabu cha Exeter na kituo cha Ekolojia na maji ardhini kilifanya utafiti huo.
Ulibaini kwamba uwezo wa muogeleaji baharini kuwa na tatizo la masikio uko juu ikilinganishwa na waogeleaji wa maeneo mengine huku matatizo ya tumbo pia yakipanda hadi asilimia 29.
Mbali na kuogelea, hatari hizo pia zinashirikisha michezo ya baharini kama vile kuteleza kwa ubao katika mawimbi.
Watafiti waliangazia tafiti 19 zinazohusiana na uogeleaji wa baharini na magonjwa kutoka Uingereza , Marekani, Australia, New Zealnd , Denmark na Norway.
Wamechanganua matokeo kutoka kwa zaidi ya watu 120,000.
Hata hivyo mtafiti mshauri Dkt. Will Gaze alisema: "Hatutaki kuwazuia watu kwenda baharini, suala ambalo lina manufaa mengi ya kiafya kama vile kuimarisha maungo.Hatahivyo ni muhimu kwamba watu wanajua athari zake ili waweze kufanya uamuzi.
Dkt Gaze amesema kwamba watu wengi hupona magonjwa hayo bila kupata tiba yoyote lakini yanaweza kuwa mabaya kwa watu wasio na kinga nzuri kama vile watu wazee na watoto.
Aliongezea: Tumetoka mbali sana katika kusafisha maji yetu, lakini ushahidi tulionao unaonyesha kuna kazi kubwa ya kufanywa.Tunatumai utafiti huu utachangia juhudu zaidi kusafisha pwani zetu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search