Zaidi ya walimu 800 wahitajika Zanzibar...soma habari kamili na matukio360...#share

ZAIDI ya walimu 800 wanahitajika katika shule mbali mbali
visiwani Zanzibar ili kupunguza uhaba wa walimu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amalia Zanzibar, Riziki Pembe Juma
Hayo yameelezwa na katibu mkuu wa chama cha walimu Zanzibar (ZATU) Mussa Omar Tafurwa katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Amesema mfumo wa elimu unakabiliwa na changamoto nyingi
ikiwemo upungufu wa walimu, vifaa vya kusomeshea na uhaba wa madarasa.
Amesema hali ni mbaya zaidi kisiwani Pemba na kwa Unguja ni kwa baadhi ya mikoa ya Kaskazini na Kusini.
“Upungufu wa walimu upo kama tulivyosema kisiwani Pemba tu
utafiti utulioufanya ndani ya chama chetu walimu wanaohitajika
ni zaidi ya 800," amesema.
Kuhusu upungufu wa vifaa vya kusomeshea amesema imetokea baada kusitishwa michango.
Hivyo ameomba kutengwa fungu la fedha kwa ajili ya shule ili kukidhi hali halisi ya upungufu huo wa fedha katika shule .
Akizungumzia kuhusu upungufu wa madarasa amesema hali ilivyosasa ni
msongamano mkubwa wa wanafunzi na kwamba darasa linawafunzi kati 70-100. Ingawa hali hiyo imekuwa ikionekana kuwa ni ya kawaida.
No comments:
Post a Comment