NEC waikana Chadema.... soma habari kamili na matukio360..#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imesema hadi sasa haijapokea malalamiko yoyote kutoka chama cha Chadema inayohusu  watendaji walioteuliwa na tume kusimamia uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni .

Pia imevitaka vyama vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa madiwani na ubunge kuzingatia kipengele cha 2.1(d)(iv)  cha maadili ya uchaguzi kuwa ni kosa la kimaadili kueneza taarifa ambazo si sahihi kuhusiana na mchakato wa uchaguzi.


Ramadhani Kailima

Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima amesema hayo leo jijini Dar es Salaam.

"NEC inawafahamisha Chadema na umma kwa ujumla, kuzingatia matakwa ya kanuni ya 21 ya kanuni za uboreshaji wa daftari kudumu la wapiga kura ya mwaka 2018 kama ilivyorekebishwa mwaka 2014 ikisomwa pamoja na kipengele cha 9.2(c) cha Kitabu cha Maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi ya mwaka 2015,"amesema.

Amesema Chadema ilidai tume imehamisha vituo 46 vya kupigia kura katika kata tatu za Kigogo, Mwananyamala na Kijitonyama bila kuwashirikisha  na kufafanua kuwa vituo vya kupigia kura havitakiwi kuwa kwenye maeneo ya kanisa, misikiti, nyumba za viongozi au mashabiki wa vyama vya siasa, kambi za jeshi na polisi.

"Katika kikao kilichoshirikisha wawakilishi 16,Chadema kiliwakilishwa na mwenyekiti wilaya ya Kinondoni Mustapha Muro na Katibu Shabani Kirita...Chadema ilikuwa ni sehemu ya maamuzi ya kukubali kuhamishwa vituo, "amesema.

Kailima amesema ni wajibu wa vyama siasa na viongozi wa vyama vya siasa na wagombea kuhakikisha wanaheshimu na kuzingatia maadili ya uchaguzi na wawaelimishe wanachama, wafuasi na wapenzi  kuheshimu sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi au sheria na kanuni zingine za nchi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search