20 kutoa ushahidi dhidi ya Madabida....soma habari kamili na matukio360...#share


Na Abdulrahim Sadiki Dar es Salaam.

Mashahidi wasiopungua 20 wanatarajiwa kuanza kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano Aprili 17, 18 na 19, 2018.

Ramadhani Madabida


Hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi, washtakiwa kukumbushwa mashtaka yanayowakabili na kisha kusomewa maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro.

Madabida na wenzake wanakabiliwa na mashtaka  mawili ya kusambaza dawa bandia za kufubaza makali ya Ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, uzembe wa kuzuia kosa kutendeka na kusababisha hasara.

Mbali na Madabida  ambaye ni afisa mtendaji mkuu, washtakiwa wengine ni Seif Shamte ambaye ni mkurugenzi  wa uendeshaji,  Simon Msoffe meneja masoko na  Fatma Shango mhasibu msaidizi wote wa Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd. Pamoja na Sadick Materu na Evans Mwemezi ambao ni maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa.  
 Wakisomewa maelezo ya awali, mahakamani hapo na Wakili Kimaro, Madabida, Shamte, Msoffe na Shango wakiwa kibali maelezo yao binafsi ikiwamo majina na nafasi zao za kazi.

Pia walikubali kuwa usajili wa kuzalisha was dawa za ARV  TT-VIR 30 yenye viambata vya Stavudine 30 mg na Nevirapine 20mg na Lamivudine 150mg, ilisajiliwa na Mamlaka ya chakula na dawa TFDA.

Walikubali kuwa muonekano wa plastiki za kuhifadhia vidonge uliosajiliwa ni wakuhifadhi vidonge 60.

Waliendelea kukubali kuwa Bohari Kuu ya Dawa MSD ilikuwa ni mteja mkubwa wa hiyo kampuni ya TPI.

Machi 17,2009 MSD waliingia mkataba na TPI wa kusambaza hizo sawa za ARV na kwamba mkataba huo ilikuwa na thamani ya Sh 5, 236,845,200.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Joseph Mgaya alisaini mkataba huo kwa niaba ya MSD  na Kisah Lisha na Benjamin Kati ambao ni Mkurugenzi wa Masoko na MkurugenziMtendaji wa TPI Respectively waliingia hayo makubaliano kwa niaba ya TPI.

Washtakiwa hao waliendelea kukubali kuwa kwa kutumia mkataba huo, Machi 30, 2011 MSD waliamuru TPI kuwasambazia vikopo ,19,300 vya dawa ya ARV kwa bei ya dola za Kimarekani 155.172.

Walikubali  kwamba MSD ilitoa call of oder hiyo ambayo ilitekelezwa na Joseph Mgaya kwa niaba ya MSD na Kisah Lisha kwa niaba ya TPI na kwamba mshtakiwa was tatu alishuhudia utekelezaji wa hiyo call of oder.

Hata hivyo washtakiwa hao mashtaka mengine yote yanayowakabili waliyakataa.
Kwa upande wa washtakiwa Sadick Materu na Evans Mwamezi ambao ni maofisa wa viwango vya ubora Bohari Kuu ya Dawa(MSD) wao walikubali maelezo yao binafsi ikiwamo majina yao, nafasi zao binafsi na kwamba walishtakiwa lakini mashtaka mengine yote wameyakana.

Katika kesi hiyo Madabida,  Seif, Simon na  Fatma  wanadaiwa kuwa Aprili 5, 2011 jijini Dar es Salaam waliisambazia Bohari Kuu ya dawa MSD makopo 7776 ya  dawa bandia za ARV’s zenye mchanganyiko wa dawa ya stavudin 30mg +nevirapine 200mg+lamivudine 150mg.

Dawa hizo zilizotengezwa Machi 2011 na kuisha muda wake wa matumizi Februari 2013 huku zilionyesha kuwa ni halali wakati si kweli.

Washtakiwa hao wanadaiwa pia Februari 11,2011 waliisambazia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) makopo 4476  ya dawa hizo bandia za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi.
Wanaaendelea kudaiwa kuwa kati ya Aprili 12 na 29,2011  washtakiwa hao kwa nia ya kudanganya, walijipatia  Dola za Marekani 98,506.08  ambazo ni sawa na Sh 148,350,156 fedha hizo ni maalipo ya jumla ya makopo 12252 ya dawa hizo bandia za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi waliyoisambazia MSD.

Kwa upande wa Washtakiwa  Sadick Materu na Evans Mwemezi  wao wanadaiwa kuwa  kati ya Aprili 5 na 13 mwaka 2011 wakiwa maafisa wa Bohari Kuu ya Dawa walishindwa kuzuia kosa kutendekea.

Washtakiwa  hao wote, wanadaiwa katika kipindi hicho walishindwa kutimiza wajibu na kuisababishia MSD  kupata hasara ya Sh 148,350,156.48 kwa kusambaza dawa hizo bandia za kufubaza makali ya Ukimwi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hao walikana na wapo nje kwa dhamana

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search