Zitto atoa njia sakata la sukari nchini... soma habari kamili na matukio360....#share


Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameshauri mawaziri wa viwanda na biashara wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar kukutana ili kutatua changamoto ya katazo la sukari kutoka kiwanda cha sukari Zanzibar kuuzwa Tanzania bara.
Pia amesema ikiwa suala hilo litashindikana anaishawishi serikali ya mapinduzi  Zanzibar kuishtaki Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki kwa kukiuka itifaki ya soko la pamoja.


Ametoa msimamo huo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam na kwamba katazo hilo ni kinyume na itifaki ya muungano katika masuala ya uchumi pamoja na itifaki ya soko la pamoja kwa nchi za jumuiya ya Afrika Masharika (EAC).
“Kwa hiyo mimi nilikuwa na msihi waziri wa viwanda na biashara, akae na waziri wa viwanda na biashara wa Zanzibar watatue jambo hilo,”
“Ikishindikana naishawishi serikali ya mapinduzi  Zanzibar iishtaki serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mahakama ya Afrika mashariki kwa kukiuka itifaki ya soko la pamoja,” amesema  Zitto.
Zitto amesema haikuwa busara kwa msemaji wa serikali kujibu malalamiko hayo ya Zanzibar juu ya suala hilo ambayo yametolewa na waziri  Balozi Amina Salum Ali kwani aliyetakiwa kujibu ni Charles Mwijage waziri wa viwanda na biashara.
Hivi karibuni baada ya kuwapo kwa malalamiko hayo serikali kupitia msemaji wake mkuu Dk. Hassan Abbasi alikanusha taarifa hizo na kusema  sukari  haijazuiwa kuuzwa Tanzania Bara.
Alisema pamoja na nchi  kuungana katika masuala ya kisiasa na suala la uchumi pia ni la kimuungano hivyo bidhaa kutoka bara na visiwani zinatakiwa kusambaa kote  bila vikwazo.
Pia alisema hata kama isingekuwa hivyo kwa kuwa nchi hizi zipo katika EAC ambayo inaitifaki ya soko la pamoja bado bidhaa kutoka Zanzibar hazitakiwi kupata vikwazo vyovyote.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search