Abdul Nondo aachiwa kwa dhamana....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Iringa

MWENYEKITI wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo ameachiwa kwa dhamana leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa
Nondo ameachiwa baada ya Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, John Mpitanjia kutoa maamuzi kuwa dhamana ipo wazi na mtuhumiwa huyo kutimiza masharti ya dhamana.
Abdul Nondo
Masharti ya dhamana ni kudhaminiwa na watu wawili ambao ni wakazi wa Iringa, huku mmoja awe mfanyakazi wa serikali, na wanatakiwa waweke bondi ya Sh. 5 milioni sambamba na kuwa na mali isiyohamishika, ambayo Nondo ameyatimiza na kupata dhamana.
Kesi imehairishwa hadi Aprili 4, 2018 itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Nondo anatuhumiwa kwa makosa mawili, la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kuwa yupo hatarini.
Shitaka la pili ni kutoa taarifa za uongo kwa watumishi wa umma mjini Mafinga alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha Polisi Mafinga kuwa alitekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam na kupelekwa Kiwanda cha Pareto cha Mafinga.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search