Ajali yaua 24, yajeruhia 10 Mkuranga.... soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Mkuranga
Watu 24 wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa katika ajali baada ya gari aina ya hiace kugongana na lori katika kijiji cha kitonga wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Kibiti, Mohamed Likwata amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kwamba ajali imetokea usiku wa kuamkia leo Machi 25, baada ya hiace hiyo kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea mkoani Mtwara kuelekea Dar es salaam.
Kamanda Likwata amesema majeruhi wote wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment