Aveva alazwa ICU Muhimbili... soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu Dar es salaam
RAIS wa klabu ya Simba, Evans Aveva amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya taifa Muhimbili. Aveva anasumbuliwa na matatizo ya figo.
Evans Aveva kushoto akiwa na Godfrey Nyange 'Kaburu'
Hayo yameelezwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri na wakili anayewatetea, Evodius Mtawala wakati kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo.
" Mshtakiwa wa kwanza Aveva, tangu jana amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi hali yake siyo nzuri" Alieleza Wakili Mtawala mahakamani hapo.
Hata hivyo,Mwendesha Mashtaka wa Takukuru,Leonard Swai naye aliiambia mahakama kuwa Aveva ni mgonjwa na kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo,Wakili Mtawala aliiambia mahakama kuwa walizungumza na upande wa mashtaka na kuelezwa jalada la kesi hiyo bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na wameomba wapewe siku 14 ili waweze kueleza kitu.
Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 22,2018.
Wakati kesi hiyo ikitajwa mahakamani hapo alikuwapo makamu wa rais wa Klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu'
Washtakiwa hao wanakabiliwa na Mashtaka matano ya uhujumu uchumi ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha wa Dola za Marekani (USD) 300,000.
Washtakiwa hao wapo mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment