Balozi wa Sweeden afungua maonesho ya picha...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
BALOZI wa Sweeden
nchini Katarina Rangnitt amefungua maonesho ya picha yanayoonesha jinsi wazazi
wa kiume wa Tanzania na Uturuki wanavyoshiriki katika malezi ya watoto.
Balozi wa Sweeden nchini, Katarina Rangnitt akizungumza alipokuwa akizindua maonyesho ya picha yanayoonesha jinsi wazazi wa kiume wa Tanzania na Sweeden wanavyoshiriki katika malezi ya mtoto Coco beach jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye
ufunguzi huo uliofanyika jana Coco beach jijini Dar es Salaam, Rangnitt amesema
lengo la maonesho hayo ni kuonesha umuhimu wa wanaume kushiiki katika malezi ya
mtoto na kuhamasisha usawa wa kijinsia.
“Ushiriki wa mwanaume
kama baba kwenye malezi ya mtoto unaumuhimu mkubwa kwenye maisha ya wanawake,
lakini pia unaleta matokeo chanya kwa wanaume wenyewe,” amesema.
Amesema kuwa kwa
Sweeden kumepigwa hatua kubwa katika ushiriki kwani wanaume hupewa hata likizo
ya uzazi pale wake zao wanapojifungua.
Ameongeza kwamba, baba
anapokuwa karibu na familia kabla, wakati na baada ya mtoto kuzaliwa inasaidia
kuwa na matokeo chanya katika afya ya mama na mtoto, mama na mtoto hupata msaada
wa muda mrefu katika huduma mbalimbali, lakini pia na kuwa na mchango
chanya katika makuzi ya mtoto kiafya na
kiakili.
Maonesho hayo ni ya
siku sita na kilele chake ni Machi 21, 2018.
Baaadhi ya wazazi walioshiriki katika uzinduzi huo akiwemo msanii wa filamu za kitanzania 'Bongo movie' Singo Mtambalike (wapili kutoka kushoto) wakielezea jinsi wanavyoshiriki katika malezi ya watoto kwenye familia zao.
Baadhi ya watu waliohudhuria kwenye ufunguzi huo
Baadhi ya watu waliohudhuria kwenye ufunguzi huo
No comments:
Post a Comment