Ushirika watoa tani 120 za saruji ujenzi ofisi walimu.... soma habari kamili na matukio360....#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda  amepokea tani 120 za mifuko ya saruji sawa na mifuko 2,400  kutoka kwa vyama vya ushirika 27 vya mkoa huo vilivyoguswa na kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam.
Ushirika wakimkabidhi tani 120 za saruji mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda

Mifuko hiyo  ina uwezo wa kufyatua tofali 70,000  zitakazojenga ofisi 14 za kisasa za walimu.

Akipokea mifuko hiyo jana Makonda amesema shughuli ya ujenzi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri  na amewashukuru wadau  wanaoendelea kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Dar es salaam, Tumaini Wilfred amesema wameguswa na jitiada zinazofanywa na  Makonda katika  kuboresha mazingira ya walimu  na kuwa ni jambojema linalolenga kuleta ukombozi wa fikra.

 Tumaini amesema Ushirika utaendelea kuunga mkono kwa kila hali juhudi zinazifanywa na Makonda.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search