Bashe ataka iundwe kamati kuchunguza usalama wa nchi... soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Nzega Mjini (CCM) Hussein Bashe amewasilisha kwa katibu wa bunge barua ya kusudio la
kuundwa kamati teule kuchunguza matukio yanayoonesha kutishia umoja, usalama na
mshikamano nchini.
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe.
Kupitia ukurasa wake
wa Twitter Bashe ameandika “Leo asubuhi
nimewasilisha Kwa Katibu wa Bunge barua ya kusudio la kuwasilisha Hoja Binafsi
ya kuunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza matukio mbalimbali yanayoonesha
kutishia umoja, usalama na mshikamano wa Taifa letu,”.
No comments:
Post a Comment