Dk Aman Kabourou afariki dunia .... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu

MBUNGE mstaafu wa Kigoma Mjini, Dk Aman Walid Kabourou amefariki Dunia Machi 06-2018 usiku.

Dk Aman Kabourou 

Taarifa zinaeleza Dk Kabourou alifikishwa   Hospitali ya Taifa Muhimbili Machi 4-2018 akitokea Hospitali ya Mkoa wa Kigoma. Alifikishwa MNH saa 13:00 mchana.

Mbunge  wa sasa wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe katika ukurasa wa  facebook ameandika;

Katika miaka ya 1995  hadi 2005 Kabouroua alikuwa ni miongoni wa wanasiasa walioimarisha upinzani nchini.

Mbali na ubunge wa Kigoma mjini kupitia Chadema, aliwahi kuwa mbunge wa Afrika Mashariki kupitia CCM.

Pia aliwahi kuwa naibu katibu mkuu bara wa Chadema. Vile vile  aliwahi kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma.


Mwaka 2015 aligombea ubunge jimbo la kigoma mjini kupitia CCM

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search