Grace Mugabe achunguzwa kwa kashfa....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa

Maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wamethibitisha kwamba wanafanya uchunguzi baada ya kupokea ripoti kwamba mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe amekuwa akisafirisha pembe za ndovu.
Grace Mugabe

Vyombo vya habari vya serikali vinasema kuwa mamlaka ya wanyama pori nchini humo ilifichua kwamba Grace Mugabe kinyume na sheria alisafirisha kiwango kikubwa cha pembe za ndovu hadi China, Marekani na UAE .
Mpiga picha mmoja wa wanyama pori Adrian Steiirn alisema kuwa alipata thibitisho la kashfa ya usafirishaji pembe hizo zinazohusishwa na bi Grace Mugabe baada ya kufanya kazi kama jasusi nchini Zimbabwe.
Inadaiwa kwamba Bi Mugabe alifanikiwa kusafirisha pembe hizo kupitia uwanja wa ndege wa taifa hilo bila kufanyiwa ukaguzi wowote.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search