Jacob Zuma kukabiliwa na mashtaka 16....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepatikana na mashtaka 16 ya rushwa inayohusishwa na mamilioni ya dola yaliotumika katika mpango wa silaha.
Mashtaka hayo ambayo Zuma amekataa kuhusika yanajumuisha udanganyifu aliofanya ili kujipatia fedha na utakatishaji wa fedha.
Mwezi uliopita Zuma mwenye umri wa miaka 75,chama chake cha ANC kilimlazimisha kuachia madaraka yake ya urais.
Zuma alipigiwa kura ya kutoamaniwa mara tisa katika bunge kabla hajaachia ngazi.
Mwendesha mashtaka mkuu Shaun Abraham amesema anaamini kuwa kuna sababu ya kuwa na mtazamo chanya juu ya hukumu ya kesi hii.
Msambazaji wa silaha kutoka Ufaransa Thales yeye pia atakabaliwa na mashtaka .Taarifa kutoka AFP zinasema Thales amekataa kuongea chochote kuhusu suala hilo.
Zuma anatuhumiwa kutaka rushwa kutoka kwa Thales kwa nia ya kuboresha maisha yake ya kifahari.Mshauri wake wa fedha wakati huo alikutwa na hatia ya kuomba rushwa hizo mwaka 2005 na Zuma alimfukuza kazi yake ya usaidizi wa rais.
Mashtaka ya awali dhidi ya Zuma yalikuwa yameondolewa muda mfupi kabla ya kuwa rais mwaka 2009.
Kwa sasa anakabiliana na shitaka moja la kusababisha ghasia,mashtaka mawili ya rushwa,shtaka moja la rushwa na mashtaka 12 ya udanganyifu.
No comments:
Post a Comment