Makonda:Wasanii mpo huru Dar es salaam.....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa kibali cha kuruhusiwa wasanii nchini kurekodi video na filamu eneo lolote wanalotaka ili kutangaza  vivutio vya utalii jijini humo.


Pia  amepiga  marufuku kwa watendaji wanaozuia wasanii kurekodi video za nyimbo au filamu kwenye mandhari (location) mbalimbali za jiji hilo kwa kuwa   inalorudisha nyuma utalii.



Waziri wa TAMISEMI, Sulemani Jaffo (kushoto) akizungumza na  Paul Makonda

Agizo hilo ametoa jana jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa kutangaza  vivutio vya utalii katika jiji hilo. Mgeni rasmi alikuwa ni waziri wa Tamisemi, Sulemani Jaffo

"Haiwezekani msanii akitaka kurekodi Video au Movie kwenye mitaro ya maji machafu ambayo inatoa taswira mbaya kwa jiji letu hasumbuliwi vibali lakini akirekodi kwenye Hotel, Majengo Marefu, fukwe au kwenye mazingira mazuri anasumbuliwa kibali,  hili haliwezekani, kuanzia sasa wasanii mtarekodi Video Location yoyote mnayotaka isipokuwa Ikulu, Mahakama, Maeneo ya jeshi na vituo vya polisi ambapo panahitaji vibali maalumu,"  alisema Makonda.

 Amesema lengo lake mi kuona wasanii wanapewa fursa ya kutangaza vivutio vya utalii kupitia kazi za sanaa wanazokabiliana.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search