Kesi ofisa TRA anaedaiwa kumiliki gari 19 kusikilizwa Aprili...soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu, Dar es Salaam. 


KESI inayomkabili, Afisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi anayekabiliwa  kukutwa akimiliki mali isiyolingana na kipato chake halali ikiwamo magari 19 itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 9,2018.
 Jennifer Mushi akiwa mahakamani
Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter ameeleza kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi ilipaswa kuanza kusikilizwa leo lakini mashahidi wa upande wa mashtaka waliotarajia wafike mahakamani hapo kutoa ushahidi ni watumishi wa umma na  wamepangiwa majukumu mengine na waajiri wao, wameomba udhuru.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, kesi imeahirishwa hadi Aprili 9,2018 ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.
Awali Jennifer  akisomewa maelezo ya awali alikubali kuwa yeye ni mtumishi wa TRA,aliajiriwa 2011 kama Afisa Forodha Msaidizi na majukumu yake ni kufanya upembuzi na uhakiki wa makadirio ya kodi wa bidhaa zinazoingizwa nchini na kusafirishwa nje.
Mshahara wake ulikuwa ni Sh 800,000 ambao mwaka 2016  uliongezeka hadi Sh 1,190,700.
Akisomewa maelezo hayo ya awali, Jennifer alikubali kuwa kupitia nafasi yake alitakiwa kila mwaka kueleza kipato chake na mali alizopata na kwamba alichotangaza kinaonesha yeye hana biashara wala chanzo kingine halali cha mapato zaidi ya ajira yake.
Alikataa kuwa katika  kipindi chote akiwa TRA kuanzia Julai 2011 hadi Machi 2016 alijipatia kipato cha jumla ya Sh 56,747,365 kama mshahara na marupurupu mengine.
Akiendelea kusomewa maelezo hayo ya awali, Jennifer alikana kumiliki gari 19, ambayo anadaiwa kuyaingiza nchini toka nchini Japan yenye thamani ya Sh 197,601,207 isiyolingana na kipato chake halali.
Alikana kuwa anamiliki Ardhi,Viwanja ambavyo anadaiwa kuvinunua kwa nyakati tofauti  akiwa mtumishi TRA ikiwamo plot namba 2263 block B Kimbiji Kigamboni chenye thamani ya Sh 8.4 milioni.
Shamba ekari moja lililopo Mabwepande lenye thamani ya Sh 700,000 na kiwanja kingine chenye thamani ya Sh milioni 1.7  kilichopo Bunju.
Akiendelea kusomewa maelezo hayo ya awali na Wakili Vitalis Peter,Jennifer alikubali kuwa anamiliki akaunti  katika Benki ya CRDB ila alikana kuwa katika kipindi cha Julai 2011 na Machi 2016 alifanya miamala katika Benki hiyo yenye jumla ya Sh 310, 993,647.33.
Jennifer alikubali kumiliki namba ya tigo 0713691006 ila alikataa kuwa Machi 21,2012 na Machi 30,2016 alifanya miamala kwenye namba hiyo ya Sh 1,632,915,485.
Hata hivyo alikubali kuwa anamiliki shule mbili za awali Active Tot's Zone zilizopo maeneo ya Kinyerezi na Mikocheni Dar es Salaam ila alikataa kuwa shule hizo zilisajiliwa 2014 na 2016, zinathamani ya Sh 65, 063,751.11 na kwamba  mwaka 2015 shule hizo zilimpatia mapato ya Sh ,6,212,800.
Jennifer alikataa kuwa miamala aliyoifanya kupitia Benki na tigo pesa kwa kununua vifaa vya shule, kulipia bima za magari 19, kununua viwanja na kufanya maingizo na kuondoa fedha Benki yenye thamani ya Sh 333,255,556.24.
Wakili huyo wa Serikali Mkuu alidai kuwa fedha hizo na mali anazomiliki mshtakiwa huyo hazilingani na kipato chake halali na hivyo hawezi kuelezea utajiri aliokuwa nao.

Jennifer ameshtakiwa mahakama ni hapo, chini ya kifungu cha 27, (1) (a) na (b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11ya mwaka 2007.
Katika kesi hiyo mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa  kati ya Machi 21,2016 na Juni 30,2016  jijini Dar es Salaam  akiwa  mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akimili magari 19.

Nagari hayo ni   Toyota RAV4, Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Viz, Suzuki Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish, Toyota Mark II, Toyota Wish na  Toyota Mark X.

Mengine ni Toyota Regiusage, Toyota Estimated, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown,  Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Passo na Suzuki Carry yote yakiwa na thamani ya Sh 197,601,207 Mali ambayo hailingani na kipato chake halali.

Anadaiwa kuwa, kati ya Machi  21 ,2012 na  Machi 30,2016 Dares Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akiishi maisha ya kifahari  yenye thamani ya Sh 333,255,556.24 fedha ambayo hailingani na kipato chake halali.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa huyo alikana na yupo nje kwa dhamana.


I

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search