DSE: Mtaji wa kampuni katika soko la hisa wapungua....soma habari kamili na matukio360....#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UKUBWA wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko la hisa (DSE) umepungua kwa shilingi bilioni 417 kutoka shilingi Trilioni 23.1 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 22.7 wiki iliyoishia Machi 9, 2018.
Mary Kinabo
Mary Kinabo
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na DSE, inasema mauzo kwa wiki iliyoishia Machi 9, 2018 yalikuwa shilingi Milioni 518 ikilinganishwa na mauzo ya shilingi bilioni 2.9 kwa wiki iliyoishia Machi 2, 2018.
Vile vile idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa wiki iliyoishia Machi 9, 2018 ni hisa laki 6.9 ikilinganishwa na mauzo ya hisa ya milioni 2.4 kwa wiki iliyoishia Machi 2, 2018.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa kwa wiki iliyoishia Machi 9, 2018 ni Voda kwa asilimia 51,TBL kwa asilimia 18 na Soko la hisa (DSE) kwa asilimia 11.
Ongezeko hilo limetokana na kushuka kwa bei za hisa za National Media Group
(NMG) kwa asilimia 8, Kenya Commercial Bank(KCB) kwa asilimia 7 na Acacia (ACA) kwa asilimia 5.
Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani kwa wiki imeishia Machi 9, 2018 ni shilingi Trilioni 10.2 kama ya wiki iliyoishia Machi 2,2018 .
Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepungua kwa pointi 43 kutoka pointi 2,405 hadi 2,362 pointi hii ikiwa ni kutokana na kushuka kwa bei za hisa za National Media Group (NMG), Kenya Commercial Bank (KCB) Acacia Mining (ACA).
Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 3893.
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) wiki hii imebaki kwenye wastani wa pointi 5365 kama wiki iliyopita
Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imebaki kwenye wastani wa pointi 2574 kama wiki iliyopita
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kwenye wastani wa pointi 2463 kama wiki iliyopita.
Aidha mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia Machi 9, 2018 yalikuwa Shilingi bilioni 65 kutoka Shilingi Bilioni 4 wiki iliyopita Machi 2,2018.
Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na mbili (12) za serikali zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 69 kwa jumla ya gharama ya Shilingi bilioni 65
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment