Magufuli: Sitobadilika, aahidi kumega hifadhi kuwapa wananchi....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Bukombe
RAIS John Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa
hatobadilika na ataendelea kuwa yule yule katika kuwatumikia wananchi.
Pia amesema serikali itamega maeneo ya ardhi ya hifadhi
na kuwapa wananchi ili yatumike katika shughuli za maendeleo.
Ametoa msimamo huo leo alipokuwa akifungua matumizi ya
barabara ya Uyovu- Bwaga km 45 katika eneo la uyovu runzewe wilayani Bukombe mkoani Geita.
“Sitobadilika kamwe mimi ni yule yule nitaendelea
kuwatumikia watanzania wote,’’ amesema Magufuli
Kuhusu ardhi amesema hatua ya kumega ardhi ya hifadhi
ni kufuatia kuwepo kwa ongezeko la idadi ya watanzania tangu nchi kupata uhuru.
“Ni ukweli usiopingika ni lazima maeneo ya hifadhi
yamegwe na kupewa wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo hii ni kutokana
na kwamba idadi ya watanzania imeongeza maradufu tangu nchi ipate uhuru,’’ amesema Magufuli
Amewata wananchi kuwa na subra na kwamba serikali ipo
katika mchakato wa kutoa maeneo hayo.
Rais amesema kutokana na ongezeko la watu maeneo ya
kulima na ufugaji yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Akitolea mfano amesema kwa sasa matumizi ya ardhi kwa
wilaya ya Bukombe ni asilimia 40 na asilimia 60 ni hifadhi.
“Hakuna sababu ya kuandamana wala kupigana kugombea
ardhi, serikali itatoa ardhi,’’ alisisitiza.
Barabara hiyo ni kiunganishi cha mikoa ya Geita,
Shinyanga, Kigoma, Kagera pamoja na nchi ya Rwanda
No comments:
Post a Comment