Majaji kutoa uamuzi dhidi ya Rugemarila....soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu, Dar es salaam

JOPO la majaji linaloongozwa na mwenyekiti, Bernad Luanda, Batueli Mimilla na Gerald Ndika  litatoa uamuzi dhidi ya pingamizi la awali lililowasilishwa na jamhuri katika Mahakama ya Rufaa kupinga  maombi yaliyowasilishwa na James Rugemarila kukataliwa kupewa dhamana mahakama kuu



Jopo hilo limesema litatoa tarehe rasmi itakayopangwa kutoa uamuzi na pande zote mbili zitajulishwa.


Herbinder Sethi mbele na James Rugemarila nyuma wakitoka katika mahakama ya rufani


Katika maombi hàyo, upande wa jamhuri unawakilishwa na Zainabu Mango,Peter Maugo na Tumain Kweka ambapo Rugemarila alijiwakilisha mwenyewe.

Katika maombi hayo Rugemarila anaiomba mahakama ya rufaa imruhusu kufanya mabadiliko ya taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

Pia anaomba kumuunganisha mshtakiwa mwenzake katika kesi ya Economic, Harbinder Seth kama mtu muhimu katika maombi hayo na kwamba anaomba wapatiwe dhamana wakati rufaa yao inaendelea kusikilizwa. 

Upande wa jamhuri uliwasilisha pingamizi la awali na kupinga maombi hayo kwa madai yameletwa chini ya kifungu kisicho sahihi kwani hakielekezi maombi hayo ni ya jinai au madai na kuiomba mahakama iyatupilie mbali, baada ya kusikiliza pingamizi hilo mahakama imesema itawataarifu wahusika tarehe ya kutolewa kwa uamuzi huo.

Baada ya kusema hayo Rugemarila aliiomba mahakama itupilie mbali pingamizi la jamuhuri kwasababu pingamizi hilo limeletwa kwa kanuni isiyo sahihi.

Alidai pingamizi hilo halina ufafanuzi kuhusu sababu za pingamizi na kuiomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo na ataeleza kwanini amemuunganisha Seth kama mtu muhimu.   

Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za kimarekani 22, 198,544.60 na Sh, bilion 309

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search