Makonda atoa siku 30.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa siku 30 kwa wanaume waliotelekeza watoto jijini humo kuanza kuwahudumia.

Pia amesema  wataangalia utaratibu wa kufanya marekebisho sheria ya gharama za matunzo ya mtoto kwakuwa ni ndogo na haiendani na hali ya sasa.
Mke wa rais, Janeth Magufuli kulia na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kushoto wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake  Duniani Machi 8,2018


Makonda ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika siku ya wanawake Duniani na kwamba lengo ni kuleta ukombozi kwa wanawake ili kuhakikisha wakihitaji fedha ya matumizi wanapatiwa na si kupigwa, kusimangwa, kutukanwa na kudhalilishwa.

"Kama kuna baba kwenye huu Mkoa anajijua ametelekeza mtoto na hatoi fedha za matunzo akamtafute na kuanza kutoa fedha ya matunzo kwakuwa itakapofika April 09 na ikithibitika umetelekeza mtoto utachukuliwa hatua kali za kisheria,"amesema.

Amesema ametangaza vita na wanaume wanaowapa ujauzito wanawake na kuwatelekeza jambo linalosababisha ongezeko la watoto wa mitaani, wadada kufukuzwa nyumbani na wengine kulazimika kuuza uji, kukaanga Samaki,Mandazi na Vitumbua ili wapate fedha ya kuhudumia mtoto na kwa ugumu wa maisha hujikuta wanashindwa kulipa kodi ya nyumba na kufukuzwa huku mwanaume akiendelea kula starehe na kuongeza wanawake.

Picha ya pamoja

Makonda amesema kitendo cha wanaume kukwepa majukumu ya malezi na matunzo kwa mtoto imesababisha baadhi yao kutoa ujauzito, kutupa watoto na wengine kupeleka wajukuu kulelewa na wazee na kusababisha mzigo kwa familia.

Kutokana na hilo Makonda ameandaa jopo la wanasheria na maofisa Ustawi wa Jamii watakaoanza kuchukuwa hatua za kisheria kwa wanaume wanaokwepa majukumu yao kuanzia Aprili 09 mwaka huu kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Hata hivyo Makonda amesema atashirikiana na kusimama bega kwa bega na wanawake wote waliotelekezwa kudai haki zao.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search