Mfanyabiashara ahukumiwa miaka 81 jela.....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abdulrahim Sadiki, Dar es salaam
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka 81 jela mfanyabiashara Timotheo Wandiba baada ya kutiwa hatiani katika mashtaka 27 ya kujipatia fedha kwa njia udanganyigu ya Sh 2 .1 bilioni.
Mbali ya Wandiba mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wenzake wawili Dickson Okololo na Simon Efrem ambao upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo kuacha shaka.
Akisoma hukumu hiyo leo iliyoandikwa na Hakimu Joyce Minde, Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri amesema washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na makosa 82, ambapo Upande wa mashtaka uliita mashahidi 14 kutoka ushahidi kwenye kesi hiyo.
Katika makosa hayo 82, mashtaka 27 ni ya kughushi, 27 ya kutoa hati za uongo, 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na Moja la utakatishaji fedha.
Hakimu Mashauri alisema mahakama hiyo imemtia hatiani mshtakiwa Wandiba katika makosa 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka.
Katika makosa hayo 27, Hakimu Mashauri alisema katika kila kosa Wandiba atatumikia kifungo cha miaka 3 jela, mbapo jumla itakuwa ni miaka 81, lakini vifungo hivyo vitaenda sambamba atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Pia Hakimu Mashauri alisema mahakama hiyo imemuachia huru Wandiba na wenzake, Okololo na Efrem katika makosa mengine yote baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuyathibitisha pasipo kuacha shaka.
Katika kesi hiyo, washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na makosa 82 ikiwemo kughushi, utakatishaji fedha na uwasilishaji wa nyaraka za uongo.
Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambalo limemtia hatiani Wandiba, inadaiwa kati ya December 3,2012 na February 5,2013 katika jiji la Dar as Salaam alijipatia Sh2, 119,039,398.96 kutoka Benki ya Africa (BoA) kwa njia ya udanganyifu.
Pia katika makosa ya kughushi inadaiwa walilitenda February 3,2012 na January 31,2013 jijini Dar es Salaam ambapo walighushi fomu za makubaliano ya kuhamisha fedha kutoka Benki ya BoA ikionyesha akaunti ya Sogea Sauthom imeiomba benki hiyo kuilipa akaunti ya Tracom Sh 2,119,039,398.96.
Katika shtaka la utakatishaji fedha, inadaiwa walilitenda kati ya December 4,2012 na April 30, 2014 ambapo walijipatia Sh 2,119,039,398.96 kutoka akaunti ya Sogea Sauthom katika benki ya (BoA) kwenda akaunti ya Tracom NMB tawi la Ban House wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu la kosa la kughushi.
Wakati kesi hiyo ikiendeshwa washtakiwa walikuwa rumande kutokana na kukabiliwa na shtaka la kutakatisha fedha ambapo kwa mujibu wa sheria halina dhamana.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment