Polisi wabaini Abdul Nondo wa UDSM alijiteka,.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam

JESHI la Polisi limebaini kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania(TSNP), Abdul Nondo (24) alijiteka mwenyewe na alikwenda Iringa kwa mpenzi wake.



Taarifa ya kutekwa kwa Nondo alizitoa mwenyewe na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Machi 6,2018 saa sita usiku.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipozungumza na waandishi wa habari

Amesema Polisi walianza ufuatiliaji ili  kubaini ukweli wa tukio hilo na kufungua jalada la uchunguzi lenye kumbukumbu DSM/KIN/CID/P.E/51/2018.

Amesema Machi 7,2018 Polisi Kanda maalum ilipata taarifa kutoka Polisi mkoa wa Iringa kuwa mwanafunzi huyo ameonekana akiendelea na shughuli zake na wala hakuripoti tukio la kutekwa katika kituo chochote cha Polisi.

"Jeshi la Polisi limebaini kuwa mwanafunzi huyo hakutekwa bali alijiteka mwenyewe ili kutafuta umaarufu wa kisiasa na kusababisha kuzua tafrani kwa jamii, "amesema.

Amesema baada ya kuchunguza mawasiliano yake ya simu kitaalamu kipindi chote alichojiteka, Nondo alikwenda kwa mpenzi wake aliyekuwa akifanya mawasiliano naye mara kwa mara akiwa njiani kuelekea Iringa.

Mambosasa amefafanua kuwa baada ya kupatikana walimpeleka hospitali ya rufaa Iringa kupimwa ambapo alibainika hakupewa kinywaji au dawa zozote ya kupoteza fahamu huku akionekana mwenye afya njema akiwa hana majeraha mwilini.

Amesema jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Polisi mkoa Iringa limebaini na kujiridhisha kuwa Nondo alikuwa huru nakwamba jeshi la Polisi litamchukulia hatua kwa kumfikisha mahakamani.

"Jeshi la Polisi Kanda Maalum, linatoa onyo kali na kutomvumilia mtu yeyote ambaye atajitafutia umaarufu ambao unaweza kusababisha uvunjifu wa amani katika jamii, "amesema.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search