Mmiliki TP Mazembe aanzisha chama cha siasa.... soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa
Mfanyabiashara maarufu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) na mmiliki wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi ambaye sasa amejitosa kwenye ulingo wa siasa, anazindua chama chake akiwa nchini Afrika Kusini.

Katumbi ni kiongozi wa upinzani ambaye yupo uhamishoni kutoka DR Congo baada ya kutengana na Rais Joseph Kabila.
Katumbi ambaye amewahi kuwa Gavana wa jimbo tajiri zaidi nchini humo la Katanga alijiuzulu na kumshtumu rais Kabila kwa uongozi duni.
Moise Katumbi ni kiongozi wa pekee wa upinzani nchini Congo ambaye ana ushawishi mkubwa na ufuasi mkubwa miongoni mwa raia wa Congo na anayetarajiwa kumpa rais Kabila ushindani mkali endapo atawania tena.
Alitangaza kutaka kuwania urais mwaka 2016, kabla ya uchaguzi huo kuahirishwa.
Katumbi aliondoka DRC Mwezi Mei mwaka 2016 na kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu punde tu aliposhutumiwa kuwaajiri wapiganaji. 
Baada ya hapo alihukumiwa bila yeye kuwepo kwa kuuza maeneo kinyume cha sheria na kupatiwa kifungo cha miaka 3 jela
Anakanusha tuhuma hizo na amewahi kusema kuwa bado anataka kuwania urais katika uchaguzi utakaofuata. 
 Katumbi pia ni Rais wa klabu ya soka maarufu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ya TP Mazembe.

Historia ya Katumbi

  • Jina lake la mwisho ni Tshapwe
  • Anajulikana kama Moses Katumbi nchini Zambia, ambapo aliishi kwa miaka mingi
  • Tarehe ya kuzaliwa 28 Disemba 1964
  • Eneo la kuzaliwa ni Kashobwe
  • Ni kabila la Babemba
  • Ni kaka wa kambo wa Katebe Katoto, maarufu kama Rafael Soriano, na mfuasi wa Laurent Nkunda
  • Baba yake ni Padre Nissim Soriano, Mitaliano Myahudi kutoka Rhodes
  • Mama yake ni Virginie Katumbi, kutoka familia ya kifalme ya Kazembe
  • Rais wa kablu ya Soka TP Mazembe Football iliopo Lubumbashi
  • Anajullikana kwa mapenzi yake na kofia za mtindo 'Cowboy'

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search