Ninje atangazwa kocha Ngorongoro Heroes...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limemtangaza kwa
muda, Ammy Ninje, kuwa Kocha wa muda wa Timu ya taifa ya Vijana wenye chini ya
miaka 20, Ngorongoro Heroes.
Ninje ametangazwa leo na TFF ilikuiandaa timu hiyo kwa ajili
ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya
Morocco na Msumbiji ikiwa ni kabla ya kucheza na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo kuelekea AFCON U20.
Ngorogoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Vijana ya
Morocco Jumamosi ya Machi 17, 2018 na dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana
Msumbiji, Jumatano Machi 21, 2018 ambapo michezo hiyo itachezwa katika dimba la
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON U20, Ngorogoro
Heroes itacheza dhidi ya DR Congo Machi 31 katika uwanja wa Taifa, na mchezo wa
marudiano utachezwa baada ya wiki mbili jijini Kinshansha Congo.
No comments:
Post a Comment