Rais ajiuzulu akituhumiwa kufanya matumizi binafsi....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa

Rais wa Mauritian Ameenah Gurib-Fakim amekubali kuachia madaraka baada ya kutuhumiwa kutumia kadi ya benki yenye thamani ya dola za kimarekani elfu kumi iliyotolewa na shirika la msaada katika matumizi yake binafsi.
Ameenah Gurib-Fakim
Rais huyo ataachia madaraka yake baada ya madhimisho ya miaka hamsini ya uhuru wa ya taifa lake wiki ijayo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Reuters,rais huyo amekana kosa hilo na kudai kuwa alirudisha fedha zote.
Rais huyo aliyeingia madarakani mwaka 2015 alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa nchini Mauritius.ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kwenye madhimisho ya Marais wa Mauritus.
Waziri mkuu wa nchi hiyo Pravind Jugnauth amewaambia waandishi wa habari kuwa rais Ameenah ataachia wadhifa wake kama ilivyopanga na kuongeza kwa kusema kuwa kipaumbele cha taifa hilo ndio kilichozingatiwa ili taifa hilo liendele kuwa nchi ya mfano.
Hata hivyo gazeti moja nchini humo lilichapisha uthibitisho wa nakala ambazo rais huyo alifanyia manunuzi ya vitu vyake vya thamani nchini Uingereza.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search