Roma, Pretykind wafutiwa adhabu...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandisi Wetu, Dar es Salaam

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza, leo wametangaza kufuta adhabu ya kufungia wasanii wa  muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki na Suzan Michael maarufu kama Pretykind.

Itakumbukwa hivi karibu Naibu wa waziri Juliana Shonza alitangaza adhabu ya kumfungia kwa miezi sita Roma kutojihusisha na muziki.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam Waziri Mwakyembe amesema kuwa muda wowote kuanzia sasa Roma Mkatoliki atakuwa huru kufanya shughuli zake za muziki kama ilivyokuwa awali kwa sharti moja la kukamilisha taratibu za kujisajili BASATA.

Kwa upande mwingine, Roma Mkatoliki ambaye naye aliongozana na Waziri Mwakyembe amesema kuwa hata kama ameachiwa huru lakini wimbo wake wa kibamia ataviomba vituo vya redio na runinga kutocheza wimbo huo.

Mwanzoni mwa mwezi Machi serikali kupitia Wizara ya Habari ilitangaza kumfungia miezi sita msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na masuala ya muziki kwa kukaidi amri ya kubadilisha baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa Kiba100.

Suzan Michael maarufu kama Pretykind naye alipewa nafasi ya kuongea na wanahabari ambapo alitoa pongezi kwa serikali kwa kumfundisha malezi mema na kuwaasa wasanii wenzake kuwa na tabia nzuri.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search