Romario de Souza kuwania ugavana..... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
Seneta wa Brazil na mchezaji wa zamani Romario de Souza atawania wadhfa wa ugavana wa Rio de Janeiro mwezi Oktoba.
Jimbo hilo limekumbwa na ghasia na liko katika hatari ya kufilisika.

Romario de Souza 
Mshindi huyo wa kombe la dunia la mwaka 1994 anayejulikana kama Romario anasema kuwa kampeni yake itaangazia kukabiliana na matatizo hayo.

Atakuwa mgombea wa chama cha mrengo wa kati cha Podemos. Amesifiwa kuwa seneta katika vita vyake dhidi ya ufisadi katika kandanda.
''Katika wakati huu wa ghasia, mabadiliko yanahitajika haraka. Rio ilikuwa na matatizo ya kiusalama, lakini sio kama sasa'' , mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 52 alisema siku ya Jumamosi akitangaza kuwania wadhfa huo.
Sina uzoefu wa kusimamia. Itakuwa kutokana na majaliwa ya Mungu , kwa mara ya kwanza kuonyesha kwamba nimekuwa na fursa kuonyesha kile nilichojifunza katika maisha yangu''.
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona kwa sasa anachunguzwa kwa madai ya kuficha mali yake kwa lengo la kukwepa kulipa deni, kulingana na vyombo vya habari vya Brazil.
Amekana madai hayo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search