TRA yasimamisha wafanyakazi wawili...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Lindi


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewasimamisha kazi watumishi wake wawili mkoani Lindi, kwa kile kilichodaiwa kwenda kinyume na kanuni na miongozo ya kazi inavyowaelekeza na kutumia lugha isiyo rafiki na wateja wao (wafanyabiashara).


Uamuzi huo,umechukuliwa na Kamishina kodi ya Mapato za ndani nchini, Elijah Mwandumbya, wakati wa kikao cha pamoja kati yake na wafanyabiashara wa mkoa huo,kilichofanyika Manispaa ya Lindi baada ya kusikiliza malalamiko mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Mwandumbya amesema Taifa wamekuwa wakipata taarifa kwamba hakuna mahusiano mazuri kati watumishi hao na wafanyabiashara, hali iliyohustua uongozi na kumtuma Kamishina huyo kufika mkoani humo kupata maelezo ya kina.

Kamishina huyo wa kodi za ndani amesema (TRA)  inapitia kipindi ambacho kinahitaji kuwapatia huduma bora wateja wao ili waweze kumsaidia Rais wa nchi katika utekelezaji wake wa maendeleo kwa kuhakikisha wanazingatia Sheria, kanuni, taratibu na miongozo,kuhakikisha wanatoa huduma iliyo bora kwa walipa kodi.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search