Tetesi za soka Ulaya leo Alhamisi... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
Kocha wa Ujerumani Joachim Low, mwenye umri wa miaka 58, ndiye anayepigiwa upatu kumrithi Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal iwapo raia huyo wa Ufaransa ataondoka katika klabuhiyo msimu wa joto. (ESPN)
Joachim low
Kuna hisia miongoni mwa wachezaji wa Gunners ya kutopendelewa wanaolipwa mishahara mikubwa katika kalbu hiyo ya ligi ya England. (Times)
Kipa wa Manchester United David de Gea bado anasubiri pendekezo la mkataba mpya licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Uhispania kusalia na miezi 16 katika mkataba aliyonao sasa. (Yahoo)
Mchezaji wa Fulham Ryan Sessegnon anapendelea kuhamia Tottenham, lakini mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England kwa wachezaji wa chini ya miaka 19 anawaniwa na pande tofuati katika ligi ya England. (mirror)
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Everton Dominic Calvert-Lewin, huenda akaitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England wakati Kombe la dunia likitarajiwa msimu huu wa joto. (Mirror)
Ajenti wa mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Emre Can, 'amezuia majadiliano yote' kuhusu mustakali wa mchezaji huyo mweny umri wa miaka 24 raia wa Ujerumani. (Express)
Manchester United wanapanga mazungumzo ya mkataba mpya na mchezaji wa kiungo cha mbele mwenye umri wa miaka 22 raia wa Ufaransa Anthony Martial. (ESPN)
Matumaini ya Liverpool kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Barcelona Ivan Rakitic yameingia dosari huku mabingwa wa La Liga wakiwa na dhamira ya kuendelea kumzuia raia huyo wa Croatia (AS, kupitia Talksport)
Newcastle ndio wanaopigiwa upatu kumsajili mchezaji wa Porto mwenye umri wa miaka 36 ambaye alikuwa kipa wa Uhispania Iker Casillas katika uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Newcastle Chronicle)
Brighton, Crystal Palace na West Ham zote zinamuwani mlinzi wa Lille Ibrahim Amadou, mwenye umri wa miaka 24, ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa timu ya kimataifa ya vijana Ufaransa. (Le 10 Sport, kupitia Croydon Advertiser)
Kipa wa Liverpool Simon Mignolet yupo tayari kuondoka Anfield huku Napoli na Borussia Dortmund zote zikiwaza kumchukua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (DH )
AC Milan wanataka kumsajili mlinzi wa Porto Ivan Marcano wakati mkataba wa Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 30 ukimalizika msimu wa joto.(Calciomercato 
Mlinzi wa Sunderland Michael Ledger, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na timu ya Norway Notodden FK. (Sunderland Echo)
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Margate Jordan Chiedozie, ametimuliwa kwa kumcheka mchezaji wa timu pinzani aliyeanguka katika mechi dhidi ya Leiston. (Kent Live)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search