Viongozi 12 ACT-Wazalendo wang'atuka wajiunga CCM....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
VIONGOZI 12 katika ngazi mbalimbali wa Chama cha
ACT-Wazalendo wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam
wamejivua uanachama na kuhamia CCM wakimtuhumu Zitto
Kabwe kutoa matamko kinyume na misingi ya chama.
Aliyekuwa mwenyekiti ACT-Wazalendo mkoa wa Dar es Salaam, Ernest Kalumuna akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wengine ni viongozi ngazi mbalimbali waliohamia CCM.
Kujiondoa huko kumetangazwa leo na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam, Ernest Kalumuna alipokuwa akiongea na waandishi was habari kwa niaba ya wanachama hao 12 kuelezea sababu za kukihama chama.
“Tumeshtushwa zaidi na kauli za karibuni za kiongoz wa chama
ndugu Zitto Kabwe kuhamasisha viongozi wa Chadema wakae na kufanya maamuzi
ambayo anadai sisi tutawaunga mkono huku akimalizia kwa kusema serikali
hii ni rahisi kuiangusha,” amesema Kalumuna.
Amesema matamko hayo ni ishara kuwa kiongozi huyo amefilisika
kisiasa na kueleza kitendo cha kamati kuu ya chama kushindwa
kukutana na kutoa tamko la kupinga kauli hizo inamaana sasa chama
hakina kamati kuu na hivyo chama kinaongozwa na mtu mmoja na wapambe wake.
Amesema kwa sasa chama hicho kina hali mbaya na
hakileti matumaini ya kuwa chama mbadala kama kilivyojinasibu awali
Viongozi waliohama
Ramadhan Ramadhan- Makamu Mwenyekiti Taifa Zanzibar wa kwanza
mwanzilishi aliyeandikisha chama kwa msajili, Leopold Lucas Mahona-Naibu katibu
mkuu Bara wa kwanza wa ACT aliyeandikisha chama kwa msajili, Hudson
Mwakyambiki-Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya chama.
Wengine ni Ernest Theonest Kalumuna-Katibu wa chama mkoa wa
Dar es Salaam, Mikidadi Ramadhan Kirungi-Katibu jimbo la Ubungo, Khalfan
Sadadi-Katibu jimbo la Kibamba, Sadich Mohamed Msangi-Katibu Mwenezi Jimbo la
Kibamba.
Pia wamo Swaumu Hamisi Msipu-Mwenyekiti Ngome ya wanawake
Jimbo la Ubungo, Robert Kihiri-Mwenyekiti Ngome ya vijana jimbo la Ubungo,
Mtangi Hatibu semwanza-Mwenyekiti wa kata ya Manzese jimbo la Ubungo na mgombea
udiwani kata ya Manzese 2015 na Ally Hamis Semwanza-Katibu wa chama kata ya
Manzese jimbo la Ubungo.
No comments:
Post a Comment