Wanawake wakamatwa wakitumia jina la JK kutapeli.. soma habari kamili na matukio360...#share




Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikiria wanawake watatu kwa tuhuma za kutumia jina la rais mstaafu Jakaya Kikwete na familia yake  kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Pia linamshikilia Selemani Masoud (68) mkazi wa Yombo Kikala kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka mbalimbali za serikali ikiwemo mihuri ya kughushi, vyeti feki vya vyuo na taasisi mbalimbali za serikali.


Kamada wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa akiwa amemtazama mtuhumiwa aliyekamatwa na mihuri feki Selemani Masoud (68) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Hayo yameelezwa leo na Kamanda wa kanda hiyo SACP Lazaro Mambosasa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema jipeshi hilo lilimkamata baada ya kupata taarifa za kiintelijensia kuwa kuna kundi la watu linalojihusisha na kutengeneza vyeti feki, mihuri na nyaraka mbalimbali za serikali katika maeneo ya Yombo Kilakala.

"Makachero wa kikosi kazi cha polisi walifika eneo la nyumba ya mtuhumiwa majira ya saa 10:30 jioni na kuanza upekuzi katika nyumba ya mtuhumiwa huku wakishirikiana na uongozi wa serikali za mitaa na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na nyaraka hizo," amesema SACP Mambosasa.

Amesema mtuhumiwa alikutwa na jumla ya mihuri feki 5 na miongoni mwa mihuri hiyo ni ya Baraza la Taifa la Mitihani nchini ( NECTA), Muhuri wa VETA, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Sokoine (SUA), Muhuri wa Cancellor wa UDSM, Chuo cha NIT, Chuo cha IFM na kadhalika.

Vitu vingine vilivyokutwa ni Computer mbili aina ya Dell, keyboard mbili, mouse mbili, printer mbili, external hard disk mbili, flash disk tano, mini card reader moja, extension mbil na kadhalika.

SACP Mambosasa amesema upelelezi dhidi ya mtuhumiwa unaendelea ili kubaini mtandao mzima anaoshirikiana nao na litahakikisha linawatia mbaroni wote hata kama ni watumishi wa umma.

Katika hatua nyingine jeshi hilo linawashikilia wanawake watatu kwa tuhuma za kutumia jina la rais mstaafu Jakaya Kikwete na familia yake kwa lengo la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Watuhumiwa hao ni Mase Uledi (41), mkazi wa Kitunda, Khadija Hamis (42) mkazi wa Tabata na Mwenge Uledi (33) mkazi wa Bukoba ambao walikamatwa wakiwa na simu 11 zikiwa na laini za mitandao mbalimbali na huku wakiwa la laini nyingine 10 zisizo kuwa ndani ya simu, laini hizo zinatumika kufanikisha uhalifu huo.

Amesema watu hao wamekuwa wakitumia jina la rais Kikwete kuwashawishi watu kujipatia mkopo wa fedha kwa kujitangaza kupitia ukurasa wa facebook uitwao Jakaya Kikwete Focus Vicoba, Salma Kikwete Focus Vicoba na Ridhiwani Kikwete Focus Vicoba.








About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search