Robo fainali UEFA Liverpool Vs Man City, Madrid Vs Juventus.... soma habari kamili na matukio360...#sha

Na mashirika ya kimataifa
 TIMU mbili za Uingereza zilizobaki katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya Liverpool na Man City zitamenyana katika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Real Madrid watapambana na Juventus, Barcelona na AS Roma, Sevilla dhidi ya Bayern

Mechi za kwanza za Robo fainali zitachezwa kuanzia April 3-4 na Marudiano itakuwa kati ya April 10-11 mwaka huu




Ratiba kamili hii hapa;




Vilevile Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA leo ikiwa ni siku moja  baada ya kumalizika kwa hatua ya 16 bora ya Michuano ya Europa League wamechezesha droo ya robo fainali.

UEFA wamechezesha droo hiyo ya kupanga ratiba ya Mechi za robo fainali kuwa RB Leipzig v Marseille,Arsenal v CSKA Moscow,Atletico Madrid v Sporting Lisbon na Lazio v Salzburg

Mechi za kwanza za Robo fainali zitachezwa April 5 na Marudiano itakuwa  April 12 mwaka huu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search