Yanga yaichapa Kagera Sugar 3-0...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
TIMU ya Yanga imeendelea
kuisogelea timu ya Simba kwenye msimamo wa ligi katika mbio za kuwania ubingwa
wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuibuka na ushindia wa goli 3-0 dhidi ya Kagera
Sugar.
Mchezo huo uliochezwa
kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaa, umeshuhudiwa magoli hayo yote yakifungwa
kipindi cha pili ambapo goli la kwanza limefungwa na Ibrahim Ajibu kwa mkwaju wa penati huku la
pili likifungwa na Yusuph Mhilu na latatu Kagera Sugar wakijifunga.
Ushindi huo unaifanya
Yanga kuwa nyuma ya mtani wake wa jadi Simba kwa pointi tatu kwani Simba iko kileleni mwa
msimamo kwa pointi 46 huku Yanga ikiwa na pointi 43 huku timu zote zikiwa zimecheza mechi 20.
No comments:
Post a Comment