Zitto: Hali ya maisha imewabana watanzania.... soma habari kamili na matukio360...#share
Amendika Zitto Kabwe kuwa; " Gharama za Maisha Zinapanda, Kipato cha Watanzania Kinashuka"
- Yatokanayo na Ziara za Viongozi wa ACT Wazalendo katika Kata Mbalimbali Nchini.
Zitto akiangalia mshindi
Leo ni siku ya mwisho ya awamu ya kwanza ya ziara za Viongozi wa ACT Wazalendo, katika kata zinazoongozwa na chama chetu nchi nzima. Tuko Mvomero, mkoani Morogoro, tukitembelea Kata ya mwisho ambayo tuliaghirisha kuitembelea baada ya kukamatwa na kulazwa Polisi siku kadhaa nyuma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sera na Utafiti, ndugu Emmanuel Lazarius Mvula ameanza kuchakata data zitokanazo na kero za wananchi kwenye ziara hii, hali ya wananchi wetu ni mbaya sana. Leo nitatoa tu mfano mmoja kwenye bei ya mazao ya mifugo na Kilimo kwa kuoanisha na bei ya vifaa vya ujenzi (saruji) kati ya mwaka jana (2017) na mwaka huu (2018) katika Kata 3 tunazoziongoza.
Mwaka 2017 Mkulima wa Kata ya Tomondo, Mikese, mkoani Morogoro alipata mifuko 10 ya Saruji (cement) kwa kuuza gunia 1 tu la Mahindi (Gunia ilikuwa ni shilingi 120,000 na Mfuko mmoja wa Saruji wa kilo 50 ulikuwa ni shilingi 12,000). Mwaka 2018 Mkulima huyo huyo wa Mikese anapata mifuko ya Saruji 3.5 (mitatu na nusu tu) akiuza Gunia lake 1 la Mahindi (Gunia sasa ni shilingi 50,000 na Saruji sasa ni shilingi 14,000).
Mwaka 2017 Mkulima wa Maharagwe wa Kata ya Msambara, Kasulu, mkoani Kigoma aliuza kilo 7.5 (saba na nusu) za maharagwe na kupata Fedha za kununua mfuko mmoja wa Saruji wa kilo 50 (kilo ya Maharagwe ilikuwa shilingi 2000 na Mfuko wa Saruji ulikuwa shilingi 15,000). Mwaka 2018 Mkulima huyo huyo atapaswa kuuza kilo 14.6 za Maharagwe kupata mfuko 1 wa Saruji wa kilo 50 (sasa anauza Maharagwe 1kg kwa shilingi 1300 na Saruji mfuko mmoja wa 50kg ni shilingi 19,000).
Mwaka 2017 Mfugaji wa Kata ya Sumbugu, Misungwi, mkoani Mwanza, aliuza Ng’ombe 1 ili kununua mifuko ya 27 Saruji (Thamani ya ng’ombe mmoja ilikuwa ni shilingi 400,000/- na mfuko mmoja wa Saruji ulikuwa ni shilingi 15,000/-). Mwaka 2018 mfugaji huyo huyo anapata mifuko 9 tu kwa kuuza ng’ombe mmoja (Thamani ya Ng’ombe mmoja sasa ikiwa ni shilingi 150,000/- na mfuko mmoja wa Saruji ukiuzwa kwa shilingi 17,000/-).
Hayo ni moja tu kati ya kero nyingi tulizozipokea kutokana na ziara yetu ya kuwatembelea wananchi katika kata zinazoongozwa na ACTWazalendo. Kwa ujumla hali ya wananchi ni mbaya sana, vyuma vimekaza kweli kweli, hakuna soko la bidhaa zao kabisa, na likipatikana basi ni bei ya chini mno, huku gharama za maisha kwao zikizidi kwenda juu. Inasikitisha mno.
Akizungumza na wanamvizia
Kinachoshangaza ni kuwa vyombo karibu vyote vya Habari vipo kimya kabisa, haviyaandiki masuala haya yanayohusu WATU. Sisi ACT Wazalendo tutapaza sauti kuhusu masuala haya, na tutatoa njia mbadala ya nini kifanyike ili kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi wetu.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Ziarani Mvomero
Morogoro
Machi 13, 2018

No comments:
Post a Comment