Hatima ya wema kesi matumizi dawa za kulevya kujulikana Aprili 23...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa uamuzi kama Wema Sepetu na wenzake wawili wana kesi ya kujibu au la Aprili 23, 2018.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka na kuufunga ushahidi wao.

Machi 23, 2018 upande wa utetezi uliwasilisha hoja katika Mahakama hiyo ili waone washtakiwa hao hawana kesi ya kujibu.

Mbali na Wema, wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.
Inadaiwa  kuwa  Februari 4, 2017 katika makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Wema anadaiwa kuwa Februani Mosi, 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya  aina ya bangi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search