Kinana aongoza viongozi CCM maombolezo kifo cha Winnie Mandela...soma habari kamili na matukio360...#share


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania kutokana na kifo cha Mke wa zamani na Rais wa Afrika Kusini, Hayati Mzee Nelson Mandela, Mama Winnie Mandela aliyefariki Aprili 2, mwaka huu.

Mama Winnie Mandela ambaye pia ni Mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, amefariki jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 81. Mwanaharakati huyo anatarajiwa kuzikwa Aprili 14, mwaka huu.

Pamoja na viongozi wengine wa CCM, Kinana ameongozana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Gaudensia Kabaka, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI, Ngemela Lubinga, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi, Seif Shaban Mohamed na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka.

Advertisement

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search