Maambukizi Malaria yashuka kwa asilimia 7.3 nchini...soma habari kamili na matukio360...#share

Na
Wamjw- Kasulu Kigoma
KIWANGO cha maabukizi ya ugongwa
wa Malaria nchini kimeshuka kwa nusu zaidi kutoka asilimia 14. 4 mwaka
2015 hadi kufikia asilimia 7. 3 mwaka 2017.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa
maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika leo Wilayani Kasulu
katika Mkoa wa Kigoma.
“Katika kuhakikisha tunatokomeza
kabisa ugonjwa huo Wizara ya Afya kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) tumepokea na
kusambaza vitendanishi vya malaria (mRTD) , vipimo 21, 428, 725, dawa za mseto
dozi 12, 916, 050 kwa ajili ya maralia isiyo kali, Sindano za kutibu Malaria
kali vichupa 1, 668, 464 na vidonge vya SP dozi 6, 899, 700 kwa ajili ya tiba
kinga dhidi ya athari za malaria wakati wa ujauzito” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
ili watanzania tuendelee kutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria watanzania
wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika kutumia afua zote za kupambana na
ugonjwa huo ikiwemo kunyunyizia viuadudu vya kuua viluilui vinavyoweza kuleta
malaria.
Vilevile Waziri Ummy amesisitiza
kuwa kila Halmashauri za kila wilaya kuunda kamati zitakazohamasisha usafi wa
mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu katika kutokomeza malaria.
Sambamba na hilo Waziri Ummy
amezindua takwimu za ugonjwa wa Malaria nchini ambao umefanywa na Taasisi
ya Takwimu nchini NBS ambayo ndio Takwimu itayotumika na Serikali ya
Tanzania.
Kwa upande wake Waziri Wa
Elimu na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa atahakikisha wanafunzi
wanapambana na ugonjwa wa Malaria kwa kuweka somo la afya kwa shule zote za
msingi na sekondari nchini.
Naye Mkuu wa Mkoa Wa Kigoma
Brigedia Jenerali Mstaafu Emamanuel Maganga ametoa wito kwa wakazi wa kigoma
kutumia vyandarua kwa matumizi sahihi na siyo kinyume na hapo ikiwemo kufungia
kuku na kuvulia samaki.
Kilele cha Maadhmisho ya Malaria
kimefikia tamati leo kwa kufanyika katika wilaya ya Kasulu Mkoani kigoma ikiwa
imebeba kauli mbiu isemayo “NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?
No comments:
Post a Comment