Majaliwa ashiriki mazishi mtumishi ofisi ya waziri mkuu...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo ameshiriki
maziko ya aliyekuwa mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu marehemu Bw. Atufigwege
Mwakasege yaliyofanyika katika makaburi ya Kikuyu mjini Dodoma.
Bw. Mwakasege ambaye alihamishiwa
Ofisi ya Waziri Mkuu Februari 29, 2016 akitokea Ofisi ya Rais-TAMISEMI
amefariki dunia Aprili 23 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
ambako alikuwa amelazwa baada ya kuugua.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi,
Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama amesema kifo hicho kimeiachia
pengo kubwa kwa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na familia.
“Natumia fursa hii kutoa pole kwa
wanafamilia hususan mjane na watoto. Marehemu ameacha pengo ndani ya familia,
hivyo tumuombe Mwenyezi Mungu awape uwezo na nguvu ya kuweza kuhimili pengo
hilo.”
Marehemu Bw. Mwakasege ambaye
alizaliwa Desemba 25, 1959 katika kitongoji cha Mwanjelwa mkoani Mbeya, ameacha
mjane Bibi Judith Mwakasege pamoja na watoto wane ambao ni Henry, Joel, Eva na
Kelvin Mwakasege.
Maziko hayo pia yamehudhuriwa na Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Mama Mary Majaliwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola, Katibu
Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi, Watumishi wa
Ofisi ya Waziri Mkuu.
Share
No comments:
Post a Comment