Makonda awajibu wanaobeza kampeni ya akina mama waliotelekezwa...soma habari kamili na matukio360..#shar

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wale wote wanaosema kampeni yake ya kuwasaidia akina mama waliotelekezwa na watoto imevunja sheria, pengine wana watoto nje na wanaogopa kujitokeza.


Makonda ameyasema hayo leo Aprili 19, katika uzinduzi wa hospitali ya kisasa ya mama na mtoto iliyopo Chanika iliyojengwa kwa msaada wa Shirika Maendeleo la Kimataida la Korea (Koica).

“Eti wanasema navunja sheria, natakiwa nifanye faragha kama unataka faragha tunza mtoto. Mimi siogopi, nipo tayari kufungwa lakini kwa ajili wa kutetea haki za watoto. Pengine hao wanaosema navunja sheria wana watoto wao nje wanaogopa kujitokeza,” amesema.

Jana, Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi  akiwa bungeni alisema kampeni hiyo inaweza kuleta hali ya sintofahamu na akabainisha kuwa inapaswa kufanyika faragha na sio kama inavyofanyika sasa.

Awali, Waziri wa Afya, Jinsia, Wanawake na Watoto,  Ummy Mwalimu alisema kampeni hiyo ni sahihi ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha, lakini akasema kwa sasa inafanyika huku picha za watoto zikifichwa.

Aliyeibua hilo bungeni jana alikuwa ni mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyehoji uhalali wa kampeni hiyo na akahoji kama haivunji sheria na kuwavunjia haki wanawake na watoto.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search