Msukuma aishukia serikali kufungia wasanii...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma


MBUNGE wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma amesema kufungia nyimbo za wasanii nchini si jambo sahihi kwa maendeleo ya wasanii hao.

Akizungumza katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo waka 2018/19, Msukuma amesema wasanii nchini wanalenga soko la kimataifa, kwamba haiwezekani wapeleke video za nyimbo zao, katika soko la kimataifa, ikiwamo Marekani wakiwa wamerekodi huku wamevaa madela.

Amesema ni jambo lisiloingia akilini watu kutazama video za mwanamuziki Rihanna katika vituo mbalimbali vya televisheni, huku wahusika wakiwa wamevaa nusu utupu, huku zile za Tanzania zikifungiwa.

“Mtu kaimba wimbo mwaka mzima uliopita leo waziri unaibuka na kufungia. Huko vijijini watu wameshaipata hizo nyimbo, mnatupa taabu sana huko vijijini maana watendaji wanakamata kompyuta za watu zenye nyimbo zilizofungiwa,” amesema Msukuma.

“Msitumie muda mwingi kufungia nyimbo, tumieni muda mwingi kuwaelimisha hawa wasanii maana wanatumia muda mrefu sana kutengeneza nyimbo zao.”

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search