Kandoro afariki dunia...soma habari kamili na maukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa mkoa mstaafu Abbas Kandoro amefariki
dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Kabla ya kifo chake aliwahi
kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Arusha, Singida na Mbeya na mikoa
mingine.
Siku mbili zilizopita Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimtembelea
na kumpa pole Mkuu huyo wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro ambapo awali
alikuwa amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma kabla ya
kuhamishiwa Muhimbili DSM ambapo umauti ndipo ulipomkuta.
No comments:
Post a Comment