Serikali kupima watu wenye ukimwi baa, migodini...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto imesema katika mikakati yake ya kuwatambua wagonjwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI pamoja na TB wameazimia kutembea maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo baa, migodini na mahali penngine ili waweze kuwatambua kiurahisi.

Hayo yameelezwa na serikali ya awamu ya tano kupitia Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile leo Aprili 23, 2018 Bungeni jijini Dodoma kwenye kikao cha 15 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza kutoka kwa Mbunge Masoud Abdallah aliyetaka kufahamu serikali ina mikakati gani katika kutoa elimu maalum ambayo itaweza kuenea kwa kasi zaidi katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi zaidi.

"Serikali baada ya kuona kumekuwa na changamoto kubwa sana katika utambuzi wa makundi maalum ambayo wengi wamekuwa wakiathirika na ugonjwa wa TB na UKIMWI. 

"Hivyo tumeamua kujielekeza kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari lakini vilevile tuna mkakati mahususi wa kuwatafuta wagonjwa wa TB katika migodi sambamba na hilo tumetengeneza tumetengeneza mikakati jumuishi kati ya ugonjwa wa TB na UKIMWI", amesema Dkt. Ndugulile. 

Pamoja na hayo, Dkt. Ndugulile ameendelea kwa kusema "sasa hivi tumeanza kujielekeza mahali kwenye watu wengi ili tuweze kuwapata kwa pamoja hususani wanaume ambapo mara nyingi wanakuwa katika bar. Msishangae kutuona na sisi tunapita huko kuwaomba kufanya upimaji wa suala la ugonjwa wa UKIMWI pamoja na TB".

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kumgundua mgonjwa wa TB mapema na kumuweka katika matibabu ndio njia kuu ya kupambana na kulishinda tatizo la kifua kikuu jambo ambalo lipo kwenye mikakati ya serikali katika kufufua uwezo wa kufikia watu wote wanaohitaji huduma za TB ili kuwagundua mapema na kuwatibu kikamilifu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search