Chuo cha utalii chaandaa tamasha la siku ya taaluma…soma habari kamili na matukio360…#share


Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

CHUO Kikuu cha Taifa cha Utalii (NCT) kimeandaa tamasha la siku ya taaluma lenye ujumbe ‘Fursa za Ajira kupitia Taaluma ya Ukarimu na Utalii’.
Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Shughuli za Kitaalam Stephen Madenge akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Shughuli za Kitaalam Stephen Madenge amesema lengo la tamasha hilo ni kuufahamisha umma juu ya mafunzo na huduma zitolewazo na chuo hicho.

“Kwa kuzingatia soko, ukuaji wa sekta ya utalii na ajira za utalii nchini, chuo kimeandaa tamasha la siku ya taaluma hapa chuoni kampasi ya Bustani lenye ujumbe ‘Fursa za Ajira kupitia Taaluma ya Ukarimu na Utalii’,” amesema Madenge.

Madenge amesema kwa kutumia tamasha hilo wanafunzi wataonesha kwa vitendo uhodari wa taaluma zinazotolewa chuoni hapo ikiwa ni pamoja na live cooking, cocktail na pastry products making, wine testing and tents preparation.

Amesema pamoja na hayo kutakuwa na uwasilishwaji wa mada za ukarimu na utalii kutoka kwa wataalamu mahiri wa sekta ya ukarimu na utalii wa hapa nchini.

“Kwa ujumla tunategemea tamasha hili, liwaunganishe na kuwaleta kwa pamoja wadau mbalimbali wa chuo kama hoteli, kampuni za kitalii, banki, kampuni za mawasiliano, kampuni za vinywaji na chakula, vyombo vya habari, Balozi, Taasisi, Idara na Wizara mbalimbali, wanafunzi wa shule za sekondari, wazazi na jamii kwa ujumla,” amesema.

Mategemeo mengine ni kufahamisha umma kuhusu mafunzo na huduma zitolewazo na chuo cha taifa cha utalii, kufahamisha umma juu ya fursa zinazopatikana katika taaluma ya ukarimu na utalii na sekta zakwe kwa ujumla.

Pamoja na kuwaunganisha wahitimu/ wanafunzi wao, wadau hasa waajiri wa sekta ya ukarimu na utalii na kuwaeleza wanafunzi juu ya huduma na muendelezo wa taaluma ya ukarimu na utalii baada ya kuhitimu mafunzo yao.

Amesema kwa upande wa wadau wategemee kupata wahitimu bora watakao wapatia ajira, kuwa karibu na jamii ambapo wanategemea kuwa na washiriki 800 na kupata muda wa kuifahamisha jamii juu ya huduma wanazotoa pamoja na kusambaza vipeperushi.

Hivyo amewakaribisha watu wote na wa sekta zote kushiriki katika tamasha hilo ambapo tamasha hilo litafanyika Aprili 27, 2018.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search