The Look Company Limited yaendesha semina kwa mawakala wa Miss Tanzania...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
KAMPUNI ya The Look
Company Limited imeendesha semina kwa mawakala wa Miss Tanzania nchini ikiwa ni
mchakato wa kuanza kwa shindano hilo kwa mwaka wa 2018.
Mkurugenzi wa The Look Company Limited Basilla Mwanukuzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya mawakala wa shindano la Miss Tanzania jijini Dar es Salaam.
Semina hiyo imekuja
siku chache baada ya uzinduzi wa shindano la Miss Tanzania kwa mwaka hu, uliofanywa
na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe ambalo
litasimamiwa na kampuni hiyo.
Akizungumza leo jijini Dar
es Salaam wakati wa ufunguzi wa semina Mkurugenzi
wa kampuni hiyo ambaye pia ni mwandaaji wa shindano hilo aliyekuwa Miss
Tanzania mwaka 1998 Basilla Mwanukuzi, amesema lengo ni kuwaelimisha mawakala
hao.
“Siku ya leo tumefungua semina ya mawakala,
mawakala wetu nchi nzima ambao wao ndiyo watakaoenda kuandaa mashindano ya
mikoa na kanda,” amesema Mwanukuzi.
“Nia na madhumuni ya
semina hii ni kuwaelimisha, kwa sababu wapo ambao ni wapya, hasa kuwaelimisha
kuhusiana na mashindamo mazima ya Miss Tanzania, lakini pia wabebe maono ya The
Look Company Limited ambayo iko nayo kwa sasa ili waweze kuongea lugha moja,”
ameongeza.
Ameongeza kuwa semina
hiyo itasaidia mawakala hao watakapokwenda kutafuta warembo mikoani na kwenye kanda watulete
warembo ambao haswa watanzania wanatarajia wawe wawakilishi wao katika
mashindano ya dunia.
“Tukumbuke kwamba
mashindano ya fainali yanapokea washindi wa kutoka kwenye mikoa na kanda, kwa
hiyo ni vyema kuwaelimisha, kuwasihii na kuwaongoza matarajio kitu gani tunategemea, wao ndiyo
hasa wanaenda kutafuta Miss World,” amesema.
Mkurugenzi huyo amsema
pia ilikuwa ni kuwaelimisha waweze kufanya kazi yao kulingana na tamaduni, sheria, taratibu za
nchi na za kampuni amabyo ndiyo waandaaji.
Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza akizungumza alipokuwa akifungua semina ya mwawakala wa shindano la Miss Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa nchini (BASATA) Godfrey Mngereza amewataka
mawakala hao kuhakikisha wanasimamia shindano katika ngazi ya mkoa na kanda kwa haki ili kupata mrembo atakaeweza kufanya
vizuri katika shindano la dunia.
Miss Tanzania 2010 na wakala Genevieve Mpangala akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa semina hiyo jijini Dar es Salaam.
Naye Miss Tanzania wa
2010 Genevieve Mpangala ambaye pia ni wakala amewataka warembo kujitokeza
katika shindano hilo kwa mwaka huu ili kuweza kuwania nafasi ya kuiwakisha nchi
katika ngazi ya dunia.
Sehemu ya mawakala waliohudhuria semina hiyo

Mkurugenzi wa The Look Company Limited Basilla Manukuzi akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa semina hiyo jijini Dar es Salaam.

Ofisa kutoka BASATA akitoa semina kwa mawakala wa Miss Tanzania waliohudhuria jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment