Uhamiaji watoa ufafanuzi sakata la Nondo...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

IDARA ya Uhamiaji imesema Watanzania wote waliozaliwa kuanzia mwaka 1978 wanapaswa kuwa na cheti cha kuzaliwa.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Crispin Ngonyani amesema hayo leo Jumatatu Aprili 9, 2018 alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Ngonyani amesema hayo alipotoa ufafanuzi kuhusu maagizo yaliyotolewa na Uhamiaji kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Abdul Nondo ya kuwasilisha vyeti vya kuzaliwa vya wazazi wake, babu na bibi zake linavyoweza kutekelezwa.

"Tulimweleza Nondo na mwanasheria wake kuwa, kama hawana vyeti vya kuzaliwa wanaweza kuleta affidavit (hati ya kiapo) na hilo tulikubaliana," amesema Ngonyani.

Amesema, "Lakini kama mtu umezaliwa kuanzia mwaka 1978 kwa sheria yetu lazima uwe na cheti cha kuzaliwa na tukikuomba utapaswa kutuonyesha kwa hiyo wananchi wanapaswa kulijua hili."

Nondo ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) alihojiwa Aprili 5, 2018 kuhusu uraia wake na ametakiwa kupeleka vielelezo kuthibitisha uraia wake vikiwamo vyeti vya wazazi, bibi na babu wa pande zote


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search