Ummy atoa maagizo haya kwa waganga wakuu mikoa na wilaya juu ya matinbabu ya malaria...soma habari kamili na matukio360...#share
Na
Mwandishi Wetu, Kigoma
WAZIRI Wa
Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza Waganga
Wakuu Wa Mikoa,Wa Wilaya na Waganga Wafawidhi kuweka Matangazo katika Vituo vya
Afya, Zahanati na Hospitali kwamba huduma za upimaji na Matibu ya Malaria ni
bure na Wananchi hawatakiwi kulipia kwakuwa kuna wafadhili wanao gharamia
gharama hizo.
Maagizo
hayo aliyatoa jana Mkoani Kigoma katika Zahanati ya Mwandiga Wakati akizindua
ugawaji wa Vyandarua endelevu vyenye dawa ya Muda mrefu ,kwa Wakina Mama
wajawazito na Watoto wenye umri wa Mwaka Moja wa ushirikiano wa Serikili ya
Tanzania kupitia wizara ya afya kitengo cha kudhiti malaria na Shirika la
misaada la marekani (USAID) ambapo alipokea Malalamiko kutoka kwa Wananchi
wakidai kutozwa fedha kwaajili ya Matibabu na Wakati serikali imeagiza Zoezi
hilo ni bure.
Waziri Mwalimu alisema
Ugawaji endelevu wa Vyandarua ni mradi unaoendeshwa kwa pamoja na shirika la
JohnsHopkins Center for Communication na Vectorworks kwa ufadhili wa shirika la
misaada la Marekani (USAID) kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti
malaria Na kuratibiwa na Serikali kupitia Mradi wa Kupambana na Malaria NMCP
kwa hiyo vyandarua hivyo ni bure na Wananchi wanatakaiwa wasilipie.
Aidha alisema ofisi ya
takwimu (NBS) katika kaya mwaka 2017 zilionyesha kupungua kwa kiwango cha
Maambukizi ya Malaria hadi chini ya asilimia 10% kutokana na Mikakati
iliyowekwa na Wizara kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa Malaria.
Alisema mikakati ya
Serikali ni kuongeza kasi ya upimaji wa Malaria kwa kutumia kipimo cha (mRDT)
Hadubini na Kutumia dawa za mseto pindi wanapothibitika kuwa na Vimelea vya
malaria , kuwapatia Wajawazito Vyandarua vyenye viuatilifu ili kujikinga kuumwa
na Mbu pia kuwapatia dawa za Sp kwa kipindi maalumu wakati wa ujauzito
ilikuwakinga na madhara yatokanayo na Malaria.
"Niendelee
Kusisitiza dawa za malaria na Matibabu ni bure Wananchi hawatakii kulipia,
wafadhiri wetu wanajitoa sana kuhakikisha Suala la Malaria liishe , Waganga
wafawidhi wanatuangusha sana niombe muweke matangazo na namba za simu kwenye
vituo vya Afya iliwananchi watakao lipishwa watoe Malalamiko yao ilikuweza
kuondokana na changamoto ya Ugonjwa wa Malaria", alisema Mwalimu.
Kwa upande wake Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Vijijini , Elisha Robarti alisema zahanati hiyo
inakabiliwa na upungufu wa Watumishi wahitaji ni watumishi 15 na waliopo ni watumishi
saba hali inayopelekea Watumishi kulemewa.
Wakitoa Malalamiko yao
Wananchi waliofika kupata huduma Katika Zahanati hiyo mbele ya Mh Waziri, Lydia
Leonard alisema Wamekuwa wakitozwa shilingi 2500/= kwaajili ya Kipimo cha
Malaria na kulipa dawa wanapofika kwaajili ya Matibabu .
Alisema pamoja na kuwa na
Kadi ya bima ya Afya lakini bado wanaendelea kutozwa fedha na kumuomba Waziri
kusimamia suala hilo iliwaweze kupata Matibabu bure kama serikali inavyo
elekeza.
Hata hivyo Wananchi hao
Shukuru Issa aliomba Serikali kuwajengea Kituo cha Afya Kata ya Mwandiga pamoja
na kuboreshewa huduma Za Maji kwani maji wanayo yatumia sio salama na
Wanalazimika kutumia Kilomita 13 kufuata huduma na Waziri alitoa maelekezo kwa
halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Vijijini kuanza ujenzi wa kituo hicho kwakuwa
kata hiyo inawatu wengi na inahitajika kupata kituo cha Afya.
No comments:
Post a Comment