Yanga yavutwa shati na Singida United...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
LIGI kuu soka Tanzania Bara imeendelea
tena hii leo kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja mbalimbali huku bingwa
mtetezi klabu ya Yanga SC ikilazimishwa sare ya bao 1- 1 dhidi ya Singida
United uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Bao la Singida United likifungwa na Papy
Kambale dakika ya pili ya mchezo huo wakati Yanga SC ikisawazisha kupitia kwa
Abdalla Shaibu kunako dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza.
Yanga SC na Singi United hazijawahi
kufungana ndani ya dakika 90 toka kukutana kwao wakati kwenye michezo
mingine dimba la Mwadui Complex mjini Shinyanga. Mwadui FC 2-1 Lipuli FC,
Mbao FC 2 – 1 Njombe Mji, Standa United 1 – 3 Maji Maji,
Simba SC kesho itashuka
dimbani kuikabili Mbeya City wakati Yanga SC wakisafiri kwenda kucheza mchezo
wa kombe la Shirikisho dhidi Welayta Dicha.
No comments:
Post a Comment