CCM cha laani mauaji mdogo wa Heche...soma habari kamili na matukio36...#share

Na Mwandishi Wetu, Tarime

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara kimelaani madai ya askari polisi kumuua kwa kumchoma kisu Suguta Chacha ambaye ni ndugu wa mbunge wa Tarime vijijini (Chadema), John Heche.

Akizungumza leo mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye amesema haiwezekani raia anayekamatwa kwa tuhuma yoyote kufariki kwa kipigo au sababu yoyote isiyohusika na ugonjwa wa kawaida akiwa mikononi mwa polisi.

"Nikiwa kiongozi na rafiki wa familia nalaani kitendo kilichofanywa na askari aliyefanya tukio hili," amesema Kiboye alipotoa salaamu wakati wa ibada ya mazishi ya kijana huyo inayoendelea muda huu.

Amesema kwa nafasi yake ya uenyekiti wa mkoa, ataendelea kuwahimiza watendaji wa Serikali, vyombo na taasisi zake  kutekeleza wajibu na majukumu yao kwa weledi wakizingatia sheria, kanuni na taratibu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search