DC Hapi atoa maagizo kwa Jeshi la Polisi sakata unajisi wanafunzi St. Florence...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Hapi ameliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma za mwalimu wa kiume katika Shule ya St Florence ya jijini Dar es Salaam kudaiwa kuwanajisi wanafunzi.
Ameagiza kutafutwa na kukamatwa kwa mwalimu huyo   anayetuhumiwa kufanya vitendo hivyo ambaye tangu Machi 16, 2018 haonekani shuleni hapo.

Tangu jana jioni kumekuwa na taarifa za mwalimu mmoja wa shule hiyo kuwanajisi watoto wanne wa darasa la saba, jambo lililozua taharuki.

Mkuu huyo wa wilaya alipowasili shuleni hapo alipokewa na mwalimu mkuu,  Wilson Mwabuka huku baadhi ya walimu wakitimua mbio na kujifungia wakihofia kupigwa picha.

Akizungumza baada ya kutembelea shule hiyo, Hapi aliwataka wazazi na jamii kuwa watulivu wakati polisi wakiendelea na uchunguzi.

"Walimu, wanafunzi na watumishi wa shule ni binadamu na kila binadamu ana hulka zake ndio maana tunazo sheria kwa kuwa makosa hayawezi kutotokea. Makosa ya walimu yasichanganywe na makosa ya taasisi, tuiache taasisi iendelee kutoa elimu," amesema.

Awali,  Mwabuka alisema tayari Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi hivyo hataweza kuzungumzia jambo hilo.

Amesema tangu Machi16, 2018 mwalimu huyo hajaonekana shuleni.

"Kwa hiyo kwa sababu mimi siyo mwanasheria siwezi kuzungumza, nawaomba wazazi na jamii kusubiri polisi kwa sababu wanaendelea kufanya uchunguzi na wameshatuhoji," amesema.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search