Jaffo: Wazazi hakikisheni vijana wanu wanapata elimu ya Dini ili wawe na maadili...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
WAZIRI Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Jaffo amewataka wazazi
kuhakikisha vijana wao wanapata elimu ya Dini itakayowasaidia kukua na kuishi
katika maadili.
Kauli hiyo ameitoa leo
jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
katika Fainali ya Mashindano ya kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Afrika Mashariki
inayoandaliwa na Taasisi Almanahilul Irfan Islamic Centre.
“Niwasishii wazazi
waendelee kuwapatia elimu ya dini vijana ili kupata maadili yatakayowaongoza,
kila mtu ahakikishe na atambue kuwa ni wajibu wake kuhakikisha kijana wake
anakuwa na maadili,” amesema Jaffo.
Amesena kama watalelewa katika maadili hawataweza
kushawishiwa kuvuruga amana ya nchi na badala yake watawajibika kuilinda na
aliwapongeza wazaizi kwa kuwawizesha vijana kujifunza Qur’an.
Kwa Upande wake Makamu
wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Mohamed Gharib Bilal, amewataka viongozi wa
Dini kuendelea kuhamasisha vijana kusoma Qur’an.
Sheikh Mkuu wa Dar es
Salaam Alhad Mussa amesema lengo la kuhifadhisha Qur’an kwa vijana ni kutaka
kuwafanya waishi kwa kuakisi tabia ya Qur’an kama ilivyokuwa kwa Mtume Muhammad
(s.a.w).
“Hii inasaidia kutengeneza
vijana wenye maadili na wasio sumbua nchi, kijana anayehifadhi Qur’an atakuwa ni
kijana mwenye madili na kioo,” amesema Sheikh Mussa.
Amesema mwaka ujao shindano
hilo litaanzia katika nganzi ya kitaifa, Afrika Mashariki, Afrika na katika
ngazi ya kimataifa.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi, Zanzibar, Ayoub Mohammed Mahmoud amesema shindano hilo linalenga
kuendeleza Uislamu na umoja na aliwataka vijana wote walioshiriki katika
shindano kuyatumia vizuri mafunzo waliyopata.
Aidha aliomba shindano
hilo kutumika katika kuimarisha muungano. Lakini pia aliwataka wananchi wasio
waislamu kwa kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan kuwa na subra ili kulinda amani.
Naye mlezi wa taasisi
hiyo aliyekuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akitoa
shukurani ametoa wito kwa taasisi nyingine kujitokeza katika kusaidia
mashindano kama hayo.
Kwa upande wa shindano,
lilikuwa na makundi manne ambayo ni ya Juzuu 10, Juzuu 20, Juzuu 3 na Juzuu 30
ambapo mshindi wa kwanza ni Abubakar Mohammed Omar-Tanzania Bara, wapili ni
Amanya Adilu Ally-Uganda na watatu ni Suleman Ally Matano-Kenya.
No comments:
Post a Comment